Mwandishi
Wetu
KIWI cha
yule ni chema cha hata ulimwengu uishe. Hiyo ni methali ya Kiswahili ambayo
inajibiwa kwa Kiingereza: “The blindness of that one is his good fortune.”
Methali ina
maana sawa na mapito ya msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’, kwamba pamoja na
uchakaramu wake lakini humohumo mafanikio yake yanapatikana. Hongera zake kwa
tuzo aliyotwaa Nigeria.
Tuzo ya Lulu
ina maana ya hatua tatu ambazo amezipitia kwenye tasnia ya sanaa za maigizo
nchini. Na bila shaka, Lulu bado anaidai fedha nyingi tasnia hiyo.
SANAA KIMEO
Lulu alianza
kuigiza akiwa mtoto mdogo kabisa. Uwezo wake wa kuigiza ulionekana. Kipaji
kikubwa cha sanaa za maigizo ni ngao inayombeba Lulu tangu alipokuwa
anachipukia Kundi la Kaole Sanaa kisha michezo yao kurushwa televisheni za ITV
na baadaye TBC1.
Sanaa
ilimharibu Lulu, maana watayarishaji walimpangia maeneo ya kucheza kama mtoto
mtukutu, na waongozaji walifanya kazi yao vizuri kuhakikisha Lulu anaimudu
nafasi husika.
Wanasaikolojia
wanaeleza kuwa mtoto huharibika kwa kuona kwa macho. Lulu alikuwa kwenye kambi
za Kaole na akawa anajionea jinsi wasanii wenye umri mkubwa wakifanya mazoezi
ya uhusika wa kimapenzi, usaliti, kuumizana na ndoa.
Vilevile kwa
kuigiza tabia mbaya (mtoto mtukutu) kama alivyokuwa akiigiza, taratibu vitabia
hivyo vya kuigiza vilikuwa vikiingia kwenye mzunguko wa maisha yake na
kujitengeneza kama tabia yake halisi.
Wataalam wa
saikolojia katika somo la Problematic Psychology, wanaeleza kuhusu hatari za wasanii
kuwa watu waovu kutokana na maeneo wanayoigiza katika filamu, tamthiliya au
michezo yoyote ya kuigiza.
Ongeza
mfano; Martin Lynes, 48, aliyeigiza kama mhalifu wa kwenye nyumba za watu
katika kipindi maarufu cha maigizo nchini Australia cha Home and Away, hivi sasa
yupo matatani, akituhumiwa kumbaka mwanamke mwenye umri wa miaka 51, kumpiga na
kumuumiza.
Hapo unaweza
kuona mfano wa Lynes, yaliyomtokea Lulu na walichokisema wanasaikolojia.
SANAA NUSURA
IMPOTEZE
Kimsingi
sanaa ya Tanzania ilimkuza kuliko umri wake. Ghafla akadaiwa kuwa kwenye
uhusiano wa kimapenzi na wanaume wakubwa, yeye akiwa na umri chini ya miaka 18.
Ilikuwa
lazima iwe hivyo kwa sababu aliyaona mapenzi waziwazi akiwa kazini na
aliyatamani, ndiyo maana aliyawahi.
Na hiyo siyo
kwa Lulu tu, wasanii wengi waliopata mafanikio wakiwa na umri mdogo, hukimbilia
sana mapenzi. Bow Wow, alipokaribia miaka 18 alisema: “Nikifikisha umri wa
miaka 18 naoa, nitakuwa sina kizuizi, umri utakuwa unatosha na pesa ninayo.”
Hapa ni
kuonesha kuwa Bow Wow alikuwa anayatamani sana mapenzi kwa uhuru, na ni sawa tu
kusema alikuwa anashughulika nayo sirisiri. Alikuwa akiyaona kwa wakubwa,
viwanja akienda, akiwa katika maeneo ya kurekodia, akawa anayatamani sana.
Lulu
akaripotiaw kulewa mpaka chakali, akahusishwa na watu kadhaa kimapenzi, kifo
cha Steven Kanumba ‘The Great’ kikaondoa shaka yote ya ushiriki wake wa
kimapenzi katika umri mdogo.
Yupo mtu
ambaye anaweza kudhani kifo cha Kanumba ndiyo nusura kimpoteze Lulu, hapana!
Kifo cha Kanumba angalau kimemsaidia. Kimempunguzia ile kasi aliyokuwa nayo.
Angalau hofu imekuwepo.
Lulu tangu
ametoka jela, hajawahi kuripotiwa kulewa mpaka kuzimika akiwa viwanja. Ni
ukweli kuwa kifo cha Kanumba kimembadilisha.
SANAA SASA
INAMNG’ARISHA
Tuzo
aliyopata Nigeria anastahili. Lulu ni mkongwe japo umri wake mdogo. Ana umri
mkubwa kwenye game kuliko wasanii wengi wanaotamba kwa sasa. Na kipindi chote
amekuwa fundi wa kuigiza. Ana uwezo mkubwa!
Hatimaye
sanaa iliyomharibu, ikataka kumpoteza, sasa inamvusha boda mpaka Nigeria kisha
anabeba tuzo kwenye nchi za watu na kurudi nayo nyumbani.
Muhimu ni
kuwa anastahili kuendelea kufanya kazi nzuri kwa sababu jina analo, mashabiki
anao, kipaji anacho na fursa anazo, ni jukumu lake kuutumia muda wake wa sasa
kutengeneza fedha.
Hongera
Lulu, hongera Single Mtambalike ‘Richie’ kwa kuiwakilisha vema nchi kwenye tuzo
za Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA) 2016. Mliteuliwa na mmeshinda.
Hata Richie,
sanaa hii bado anaidai fedha nyingi maana ameitoa mbali. Amesafiri nao kuvuka
mabonde na milima. Ni haki kabisa kwa mtu ambaye amehangaikia fani yake
ikamlipa inavyotakiwa. Richie anastahili pia tuzo yake.
0 comments :
Post a Comment