Na Luqman
Maloto
KAMA wabunge
wanakula rushwa. Tazama malipo yao, daraja wanalopewa, vipi tafriki barabarani?
Mbunge
aliyesema gari la shilingi milioni 90 halifai, vipi nesi ambaye mshahara wake
wa mwezi haukidhi japo mzunguko wa wiki?
Nidhamu
hakuna kabisa. Wabunge na heshima zao wanatuhumiwa kuomba rushwa. Acha Rais
John Magufuli achukue pointi zake.
Na hapa ni
kuwa kivuli cha Rais Magufuli kinaonekana kutokana na tukio tukio la kashfa
kubwa za rushwa bungeni.
Tayari wabunge
Zitto Kabwe, Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) na Hussein Bashe, Nzega Mjini (CCM)
wamejiuzulu ujumbe wa kamati ya bunge kutokana na kashfa ya rushwa.
Uamuzi wa
Zitto na Bashe, ni kufuatia habari kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amefanya mabadiliko
ya kamati za bunge kutokana na kashfa za rushwa.
Zitto na
Bashe wamejiuzulu na kutaka uchunguzi ufanyike ili wahusika wachukuliwe hatua.
Wamekataa kuwa wajumbe kwenye kamati yenye wajumbe wenye kashfa ya rushwa.
WALIODAIWA
KUNASWA
Imeelezwa
kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Martha Mlata ameshaondolewa
kwenye nafasi hiyo. Mlata ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Singida.
Wengine ni
Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndassa wa Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, Mbunge
wa Viti Maalum (CCM), Mbeya, Mary Mwanjelwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya
Ardhi, Maliasili na Mazingira.
Wapo makamu
wenyeviti na kamati zao ambao ni Raphael Chegeni (Huduma za Maendeleo ya
Jamii), Kangi Lugola (Kamati ya Hesabu za Seikali za Mitaa ‘Laac’)
INAMPA
TURUFU MAGUFULI
Kwa nini
imekuwa mapema sana? Na mbona kashfa zimeripotiwa kwa sehemu kubwa? Jibu ni
moja tu, mabadiliko katika mfumo wa uongozi ambao Dk. Magufuli ameyaweka.
Picha ya
sasa inaonesha kuwa huko nyuma wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia kamati zao, walikuwa wakicheza mchezo wa kulinda maovu ya
mashirika ya umma.
Kwamba
wabunge kupitia kamati zao, wanabaini maovu ya mashirika ya umma, hivyo wabunge
wanaomba rushwa ili wasililipue shirika husika.
Katika moja
ya vikao vya bunge katika Bunge la 10, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini
(NCCR-Mageuzi), David Kafulila, aliwahi kuwataja wabunge wawili kumuomba rushwa
mkurugenzi mmoja wa halmashauri.
Kafulila
alisema kuwa wabunge, Omar Baduel wa Bahi na Godfrey Zambi wa Mbozi Mashariki,
wote CCM (sasa Mkuu wa Mkoa wa Lindi), walimshawishi mkurugenzi mmoja wa
halmashauri kuwapa rushwa ili wamlinde.
Wakati huo,
Kafulila, Zambi na Baduel, walikuwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (LAAC).
INA MAANISHA
NINI?
Kafulila
alizungumza bungeni waziwazi. Maana yake ni kuwa kumbe wapo wabunge ambao
huomba rushwa kwenye mashirika ili kuficha maovu.
Na kwa muda
mrefu kumekuwa na kelele kuwa wabunge hupenda baadhi ya kamati zinazohusika na
ukaguzi au usimamizi wa hesabu za mashirika ya umma na serikali kuu au ile ya
Nishati na Madini.
Mwaka 2012,
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nasari, alisema bungeni na
kupendekeza: “Mheshimiwa spika, kumekuwa na tabia ya wabunge kupendelea kamati
zenye kuhusika na mashirika makubwa, sasa ibadilishwe wale wa kamati ndogondogo
ndiyo wawe wajumbe wa kamati zenye kukimbiliwa na wengi.”
TUNAONA NINI
SASA?
Mlipuko wa
kashfa ya rushwa bungeni una maana kuwa sasa hivi mashirika ya umma na taasisi
za serikali kuu kwa jumla, zimebanwa hasa.
Hivyo,
kitendo cha mashirika ya umma na taasisi za serikali, kuripoti kwa Spika wa
Bunge, Job Ndugai kuhusu kuombwa rushwa na kamati za bunge, maana yake ni
kwamba nidhamu ya watendaji katika mashirika ya umma inaonekana.
Kwamba
mchezo wa zamani ni kuwa wabunge walikuwa wakiomba rushwa kwa mashirika ya
umma, watendaji wake kwa hofu wanatoa.
Sasa hivi
kutokana na nidhamu ambayo imekuwepo na hofu ya kutumbuliwa majibu, vilevile
ukaguzi ambao umekuwa ukifanywa, imekuwa sababu ya badala ya kutoa rushwa,
waripoti.
Na imebainishwa
kuwa kashfa ya rushwa, imebainika baada ya ukaguzi maalum kufanywa na serikali.
.
Mwaka 2012,
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi,
alimwandikia barua aliyekuwa Spika wa Bunge la 10, Anne Makinda, akimweleza
kuhusu baadhi ya wabunge kumuomba rushwa ili wasimliopue bungeni kutokana na
iliyokuwa kashfa ya mafuta ghafi kwa ajili ya mitambo ya kuzalisha umeme.
Barua hiyo ilisababisha mjadala mkubwa na
baadaye Spika Makinda aliivunja Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.
Pamoja na
kuvunja kamati, spika aliielekeza kamati ya maadili iliyokuwa chini ya Brigedia
Jenerali, Hassan Ngwilizi (aliyekuwa mbunge wa Mlalo, CCM) kufanya uchunguzi wa
kashfa hiyo.
Katika
uchunguzi huo, zilipenya taarifa kuwa baadhi wajumbe waliumbuana kwa mtindo wa
“mbona na wewe… mbona na wewe… unakumbuka na wewe.”
Baadaye
Spika Makinda alitoa onyo. Hakuna hatua za kinidhamu zilizochukuliwa baada ya
ripoti kukabidhiwa kwake. Alisema onyo kali linatosha!
Sports toto's: Sports toto's (or simply your business) - Sporting 100
ReplyDeleteAs the name suggests, the sports betting landscape is already saturated with online bookmakers, with the new iPhone 토토 사이트 추천 and iPad app,